UMASKINI NIACHE (Explicit)-Stamina Shorwebwenzi

UMASKINI NIACHE (Explicit)

时间:2021-12-07

    使用手机浏览器「扫一扫」

    在手机上保存,获得更好体验

标签
歌词

Intro

Wamemchokoza tena bwana….

Wamemchokoza bear……….

Umeskini niache..…eeh! eeh! Eeh! x3

Verse 1

Aah!..Ulimuondoa mama kipindi yupo hoi anaumwa/

Akapoteza uhai kisa pesa ya matibabu hakuna/

Wewe ndio sababu ya kuvunja ndoa ya Fatuma/

Mumewe mambo mazito haujampa pesa umeuchuna/

Niache niende bwana nimechoshwa na Maisha huku sitimbi/

Unadhani sitamani kupiga picha kidimbwi/

Nizungushe wapambe mezani tungi jingi/

Mixer kuagiza vinywaji vijavyo na cheche nyingiii/

Umeniganda aisee,umeniganda kama ruba/

Hivi we ni jinsia gani, hiv ni pisi ama mjuba/

Unanichanganya kuna muda nautamani msuba/

Unanizeesha,unanikondosha sasa si unipe tu hizo fuba/

We ndiyo sababu ya dada zangu wakae kona wanajiuza/

Na Kaka zangu wawe wezi huko buza/

Na mama zangu wakeshe kuuza vitumbumbua /

Unawatesa baba zangu kuwazugusha kwenye jua/

Chorus

Usione tabasamu usoni moyoni mimi sina furaha (eeh)

Usione napendeza nje,ndani mimi nakufa na njaa

Umaskini niache,niache,niache…. X2

Verse 2

Nimesoma kidumu ufagio Kayumba ndio nako weza/

Hivi unadhani sitamani Watoto wangu wasome fedha/

Daily kwa mganga napiga manyanga/

Nazi njia panda,ili mladi tu niweza kuupata huo mkwanja/

Nikuulize nikiwa Tajiri inakuuma nini/

Au navyoitwa mbahiri kiongozi unapata nini/

Kaka zangu bodaboda nao utawapa pesa lini/

Iseeh,tumechoka kubet tutaliwa mpaka lini/

Kwenye mapenzi,wengi tupo tu ilimradi/

Ukiitwa mpenzi na hauna pesa wewe ni mpenzi mtazamaji/

Au unafurahi nikiitwa dume suruali/

Dume nisiye na gari ,dume nisiye na maisha ya ufahari /

Mbona wenzangu unawapa marolls royce ,maprado/

Mimi nikiendesha ujue naharisha ,mbona kwangu mambo bado /

Inatosha iseeh,hembu niache niende zangu/

Nipate utajiri nikakae na maboss wenzangu/

Chorus

Usione tabasamu usoni moyoni mimi sina furaha (eeh)

Usione napendeza nje,ndani mimi nakufa na njaa

Umaskini niache,niache,niache…. X2

Verse 3

watoto wa shangazi bado ni wahudumu wa bar/

hawapendi wanachofanya sema ndio hivyo tu wana njaa/

na mjomba wangu bado ni mkataa mkaa /

mtoto wake fundi mwashi mjenzi wa majengo ya mtaa/

hivi kwa nini kazi ngumu zote za sisi maskini/

unatuona power mabula eeh!!! Dah!

Hivi kwa nini/

Maisha wanayoishi yote tunayaunda sisi/

Mijengo magari mpaka hayo maofisi/

Nachukia nikiona sura ya mbunge wangu/

Nawaambia haki ya nani nimepoteza kura yangu/

Anasinzia bungeni hatetei Maisha yangu/

Bora peke yangu mimi pekee na fuvu langu/

Chorus

Usione tabasamu usoni moyoni mimi sina furaha (eeh)

Usione napendeza nje,ndani mimi nakufa na njaa

Umaskini niache,niache,niache…. X2

Hook

Nimekuchokaaah x3

Nimekuchoka umaskini

Nimechoka……aaah

展开显示全部歌词